Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 8:05 pm

News: Zaidi ya Abiria 1,000 wamerudishiwa nauli zao baada kukosa huduma ya treni

Dar es salaam: Shirika la reli Tanzania TRL Limesema kuwa kulingana na changamoto la uchakavu wa miundombinu na Treini kutokuwa na uhakika wa usafiri limetoa ahueni kwa abiria wote watakao hitaji kurudishiwa nauli pindi Treini itakapo pata itilafu sehem yoyote ile. Hii imekuja kutokana na juhudi za serikali kuboresha miundombinu ya barabara jiji la Dar es salaam lakini jitihada hizo bado nichangamoto kwa abiria wa jiji hilo mbapo zaidi ya abiria 1000 watarudishiwa nauli zao kama fidia baada yakukosa huduma ya treni kutoka stesheni kuelekea Pugu.

hali hiyo imetokana na vifaa vya treni kupata hitilafu juzi wakati treni ikiwa inawasafirisha abiria, shirika la Reli Tanzania [TRL],Limesema litawarudishia nauli abiria ambao watahitaji kwa kuwa tayari walishatoa tamko wanaweza kufanya hivyo au kutumiatena tiketi zao kwa siku ya jana.

Ofisa Uhusiano [TRI], Midladjy Maez,amesema jumla ya mabehewa 20 ambayo yanatumika na treni hiyo kutoka stesheni hadi Pugu jana yalikubwa na adha hiyo licha ya wengi kuamua kutafuta njia mbadala ya kusafiri.