- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI UMMY AITAKA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUJIKITA KATIKA MATIBABU YA KIBINGWA
DODOMA: Serikali kupitia wizara ya afya ,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imeutaka uongozi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma kuitumia hospitali hiyo kwa matibabu ya kibingwa ili kupunguza tatizo la msongamano wa wagonjwa katika Hospitali hiyo.
Hatua hii imekuja kutokana na Hospitali hiyo kuwa na msongamano wa wagonjwa ambao walipaswa kutibiwa katika hospitali za kawaida hali inayokwamisha wahitaji wa huduma za kibingwa kushindwa kupata huduma hizo kwa wakati.
Licha ya hayo takwimu za magonjwa yasiyo ya kuambukiza zinatajwa kuwa kubwa na kusababisha ongezeko la vifo vingi ambapo kati ya vifo 100 ,vifo 60 vinatajwa kutokana na magonjwa hayo.
Hayo yamebaishwa juni 22 na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati akizindua bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Benjamini Mkapa ambayo ni ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Hospitali hiyo.
Licha ya hayo Mwalimu amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza husababisha vifo vingi duniani kote kuliko yale ya kuambukiza, na kwa bahati nzuri hospitali ya Benjamin Mkapa iliaanzishwa mahususi kutoa huduma za kibingwa .
Pamoja na hayo Mwalimu amesema Kwa takwimu za kuanzia Julai 2013 hadi Juni 2016 magonjwa ya Moyo na Figo ndiyo yalikuwa yakiongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa kutibiwa nje ya nchi na kuigharimu Serikali kiasi cha shilingi Billion 36.6.
Alifafanua kua Kati ya wagonjwa 590 waliosafirishwa na serikali 430 walienda kutibiwa moyo na 160 walienda kupandikizwa figo hivyo, kwa kuanzishwa huduma za kibingwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa kutaokoa kiasi kikubwa cha pesa na kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama na badala yake pesa hizo zitatumika kuimarisha miundombinu ya hospitali nyngine nchini.
Awali akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dk Alphonce Chandika mbali na kukiri kuwa uzinduzi wa bodi hiyo ni wa kihistoria na kwamba ni mafanikio makubwa katika huduma za kibingwa hakusita kuzitaja changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo.
Ametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa magari ya kuwasafirisha watumishi,upungufu wa watumishi, na nyumba za watumishi ambapo hulazimika kusafiri umbali mrefu wa kilomita 20 kila siku kuelekea katika hospitali hiyo.
Sambamba na hayo alisema huduma za afya za Kisasa zinagharama kubwa kwani zinahitaji uwekezaji mkubwa hasa katika ujenzi wa miundombinu kama majengo, vifaa na vifaa tiba pamoja na mifumo mbalimbali ya kiuendeshaji na TEHAMA.
Naye mwenyekiti wa bodi hiyo ya wadhamini Dk Deodatus Mtasiwa ameuomba uongozi wa hospitali hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujitoa katika kupanua na kuboresha huduma za hospitali wakati wanaendelea kutatua changamoto moja baada ya nyingine kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya afya na Wizara nyingine zenye mamlaka ya kutatua changamoto hizo.