- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MPANGO ABANWA VIKALI JUU YA AJIRA NCHINI
Dodoma: Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amebanwa vikali na Wabunge wa viti Maalumu, Mariam Msabaha (Chadema) na Kiza Mayeye (CUF) kumtaka waziri huyo kuelezea mkakati madhubuti wa kutatua uhaba wa ajira kwa vijana nchini.
Wakitoa kauli hizo leo Ijumaa Juni 22, 2018 bungeni mjini Dodoma wakati wa mjadala wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2018/19.
Mayeye amesema tatizo la ajira nchini linawafanya vijana kujiingiza katika matukio hatarishi kwa ajili ya kujitafutia riziki na kumtaka waziri huyo wakati akijibu hoja za wabunge zilizoibuliwa katika mjadala huo, kueleza mkakati wa kuwakwamua vijana. “Mnasema vijana wajiajiri, hivi kijana anawezaje kujiajiri wakati mtaji hana.
Kama mnasema kujiajiri wekeni mipango na mikakati ili vijana wajiajiri, wapeni mitaji,” amesema “Waziri Mpango katika kitabu chako cha bajeti hujaelezea ajira kwa vijana ni mkakati upi na sisi tupo katika hatari gani ya tatizo hili jambo linalowafanya vijana kukimbilia nje ya nchi kutafuta ajira.”
Amesisitiza kuwa, “wekeni mkakati wa kusaidia upatikanaji wa ajira ili kuwawezesha vijana kupata kipato, hususan akinadada ambao wanajiingiza katika njia zisizo stahili kujipatia fedha.” Kwa upande wake, Msabaha amehoji,“hizi ajira mpya ambazo mnasema zinatoka, zitatoka lini? Na hawa wanaokaimu watakaimu hadi lini na ajira hizo za Muungano zitakuwa ngapi? Tunataka kujua hizo ajira.”