- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MKUU WA TUNISIA AJIUZULU MIEZI 5 BAADA YA KUINGIA MADARAKANI
Waziri Mkuu wa Tunisia Elyes Fakhfakh amejiuzulu wadhifa wake, hii ni miezi 5 baada ya kuingia madarakani hatua ambayo inatishia mvutano wa kisiasa katika taifa hilo, wakati huu linapoendelea kukabiliwa na changamoto za kiuchumi na janga la Corona.
Kujiuzulu kwake kunakuja wakati huu chama cha Ennahdha, chenye idadi kubwa ya wabunge bungeni kuonekana kugawanyika kutokana na mgongano wa maslahi.
Rais Kais Saied amesema hatua ya Elyes Fakhfakh kujiuzulu ni kuepusha migongano na taharuki katika taasisi za serikali katika taifa hilo.
Tangu uchaguzi wa wabunge mwezi Oktoba mwaka ulipota, uhusiano kati ya Waziri Mkuu na uongozi wa chama hicho haujawa mzuri, suala ambalo wachambuzi wa siasa wanasema imechangia pakubwa kujiuzulu kwake.
Pamoja na kupata idadi kubwa ya viti bungeni, chama cha Ennahdha hakikupata idadi inayyohitajika ili kuunda serikali peke yake, na kulazimika kuingia kwenye muungano na vyama vingine ili kuunda serikali