Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 10:17 pm

NEWS: WAZIRI MKUU AFIKA KUMJULIA HALI MBOWE

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumjulia hali Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendekeo (CHADEMA) Freeman Mbowe ambaye awali alilazwa katika hospitali ya DCMC Ntyuka mkoani Dodoma kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Waziri Mkuu amemuombea kiongozi huyo uponyaji wa haraka kufuatia majeraha aliyoyapata katika tukio hilo. “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tukio la kuvamiwa kwa Mheshimiwa Mbowe na watu ambao bado hawajajulikana, namuomba Mwenyezi Mungu amjalie apone haraka ili aweze kurejea katika majukumu yake", amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Tayari Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesafirishwa kwa ndege kutoka Dodoma kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.