- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI ATAKIWA KUOMBA RADHI WANANCHI KWA KUSEMA UWONGO
Dodoma: Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ametakiwa kuwaomba radhi Watanzania wote na Bunge kwa kudanganya kuwa fedha za maendeleo zilizotolewa katika bajeti ya mwaka 2017/18 ni asilimia 56 ilhali kamati ya bunge imebaini ni asilimia 22 tu maneno hayo ameyasema Mbunge wa Monduli kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Julius Kalanga Bungeni Dodoma
Kalanga ameyasema hayo Jana Mai 7 wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma amesema takwimu nyingi za taarifa za hotuba hiyo zinapingana na za Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.
Amesema waziri huyo ameonesha fedha za miradi ya maendeleo ya maji zimetolewa kwa asilimia 56 ili kulishawishi Bunge lipitishe bajeti hiyo ilihali wilaya nyingi ikiwamo Monduli hazijatengewa bajeti za mradi wowote mwaka huu.
“Waziri anasema ni asilimia 56 wakati kamati inasema 22, tunataka kujua nani ni mkweli? Amehoji Kalanga.
Akiwasilisha bajeti ya Mhandisi Kamwele katika bajeti ya mwaka 2017/18 hadi kufikia Machi mwaka huu wizara ilipokea fedha za maendeleo Sh bilioni 347.5 sawa na asilimia 56.