Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 3:30 pm

NEWS: WAZIRI AFAFANUA KATAZO LA KULALA NA MGONJWA HOSPITALINI

Dodoma: Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt Faustine Ndungulile ametolea ufafanuzi katazo la muda mrefu la ndugu wa mgonjwa kuto kulala na mgonjwa wake katika Hospitali zetu hasa za rufaa.

Akiongea leo Mai 9, 2018 kupitia ukurasa wake wa Twitter Dkt Ndugulile ambaye pia ni Mbunge Kigamboni amesema kuwa wanakataza ndugu kulala na mgonjwa kwa sababu za kiafya ambazo ndugu asipate maambukizi kutoka kwa wagonjwa ndani ya Hospitali na mgonjwa asipate maambukizi mapya kutoka kwa anayemuuguza ambaye kimsingi anatoka njee ya hospitli.

"Taratibu za hospitali haziruhusu ndugu kulala na mgonjwa hospitalini. Lengo ni kukinga wagonjwa kupata maambukizi toka nje na ndugu kupata maambukizi toka kwa wagonjwa" amesema Naibu waziri

Ufafanuzi huo umeutoa baada ya kuwepo kwa mjadala kwenye Akaunti yake juu ya kwanini Ndugu asilale na Mgonjwa wake wakati wa kumuuguza wakizingatia kutokuwepo kwa huduma nzuri kwa wauguzi waliopo katika hospitali zetu


Pia yupo mdau aliandika ombi Rasmi kumtaka Rais Magufuli kama kunauwezekano wa kujenga jengo pale Muhimbili kama hostel kwa ajili ya watu walioleta watoto wao Muhimbili toka Mikoani? "Mkuu watu wanauguliwa wanalala stendi.. waonee huruma" aliandika mdau

Pia Dkt Ndungulile amewaomba wadau waendelee kulete ushauri juu ya ndugu wanaoleta wagonjwa kutoka njee ya mkoa wa Dar es salaam "Tunapokea ushauri wenu kuhusu huduma kwa ndugu toka nje ya mkoa. Tutalifanyia kazi" alimalizia Ndugulile