Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 2:00 am

News: Watu wenye ulemavu wa ngozi [albino] wapata neema ya mafuta

Dodoma: JUMLA ya watoto 95 wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wamepatiwa mahitaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafuta ya kupata.

Mahitaji hayo yametolewa leo katika Uzinduzi wa clinic ya kuwasaidiamahitaji ya msingi ikiwamo mafuta ya kupaka watu wenye ulemavu wa ngozi[albino] umefanyika katika hospital yarufaa ya mkoani Dodoma.

Zoezi hilo la kuwapatia mahitaji jamii ya watu wenye ulemavu ufanyika kila baada ya miezi minne zoezi hilo litakuwa endelevu .

Dk. Charles kiolongwe,ambaye ni mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma ndiye alikuwa ngeni rasm katika uzinduzi wa zoezi hilo.

Akizungumza na jamii hiyo pia aliwasisitza mambo kadhaa ambayo ni.

  • 1.watu wenye ulemavu walemavu kutumia mafuta kwa uwangalifu ni pamoja nakuzingatia muda wakupaka mafuta hayo dakika 15 kabla ya kutembea juani.
  • 2. walemavu kutoa ushirikiano katika kwenda hospitalI mara kwamara ili kucheki afya na maendeleo ya ngozi zao.