- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WATU WAWILI WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA KUJIRIPUA MASHARIKI MWA LIBYA
Afisa mmoja wa ngazi za juu wa usalama wa Libya amesema kuwa, watu wawili wameuawa mashariki mwa nchi hiyo baada ya gaidi mmoja kujiripua katika kituo cha upekuzi cha "Jeshi la Taifa la Libya" linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar.
Afisa huyo amesema kuwa, mtu mmoja alijiripua na gari alilokuwa analiendesha katika eneo lililoko umbali wa kilomita 90 mashariki mwa mji wa Sirte (kilomita 450 mashariki mwa mji mkuu Tripoli) na kusababisha vifo vya afisa mmoja wa Jeshi la Taifa la Libya na raia mmoja.
Hadi sasa hakuna mtu wala kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo ambalo limetokea siku moja baada ya Jenerali Khalifa Haftar kuanzisha operesheni ya kuukomboa mji wa Derna wa mashariki mwa Libya kutoka mikononi mwa genge moja la kigaidi.
Kundi la kigaidi linalojiita kwa jina la Baraza la Mujahidi wa Derna ambalo ni moja ya matawi ya mtandao wa al Qaida limekuwa likiushikilia mji huo wa kiistratijia kwa muda mrefu sasa.
Libya haijawahi kushuhudia utulivu tangu mwaka 2011 baada ya Marekani na madola ya Magharibi kuivamia kijeshi nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika wakati wa kampeni za kumng'oa madarakani Kanali Muammar Gaddafi.