Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 1:44 pm

NEWS: WATU 26 WAUWAWA KWA KUSHAMBULIWA KWA VIZU NA BUNDUKI BURUNDI

Bujumbura: Watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami kwa silaha wameuwa watu 26 Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Burundi.

Ripoti zinasema,mauaji haya yalitokea siku ya Ijumaa usiku, huku wenyeji wakivamiwa kwa kupigwa risasi na kuchomwa visu.

Afisa wa serikali ambaye hakutaka kutajwa, ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa amehesabu miili 23.

Waliouawa ni pamoja na wanaume, wanwake na watoto na huenda idadi ikaongezeka.

Watu wengine zaidi ya 10 wameripotiwa kujeruhiwa katika uvamizi huo huku polisi walisema kuwa wanafanya uchunguzi.


Haijafahamika watu walioptekeleza uvamizi huo ni akina nani, lakini wakaazi wa kijiji hicho katika mkoa wa Citiboke wanashuku kuwa huenda wamevuka mpaka kutka nchi jirani ya DRC.

Mauaji haya yamekuja, kuelekea zoezi la kura ya maoni tarehe 17 kuibadilisha Katiba ya nchi hiyo, kumwezesha rais Pierre Nkurunziza kuendelea kukaaa madarakani hadi mwaka 2034.

waziri wa usalama nchini humo Alain Guillaume Bunyoni alisema kuwa wale waliotekeleza shambulio hilo walikuwa ni magaidi kutoka nchini jirani ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Amesema baadhi ya waathiriwa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini ambapo wanatibiwa. Ameongezea kuwa mazungumzo yanaendelea na mamlaka ya DRC kwa lengo la kuwakamata washukiwa wakamatwe.

Walioshuhudia wanasema kuwa washambuliaji hao waliingia nyumba baada ya nyumba usiku wakiwapiga risasi watu na kuwadunga visu mbali na kuchoma nyumba zao.