- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WATU 21 WAUAWA NA KUJERUHIWA KATIKA MRIPUKO WA BOMU NCHINI SOMALIA
Polisi ya Somalia imetangaza kuwa, kwa akali watu 21 wameuawa na kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi lililotokea sokoni nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shambulizi hilo la kigaidi lilitokea jioni ya jana katika soko lenye watu wengi kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu na kwamba habari za haraka zinaeleza kuwa watu 11 walipoteza maisha eneo la tukio huku wengine 10 wakijeruhiwa. Kundi la kigaidi na ukufurishaji la ash-Shabab limetangaza kuhusika na mripuko huo. Aidha polisi imesema kuwa bado inaendelea kufanya uchunguzi wa hujuma hiyo na kwamba, baadhi ya waliojeruhiwa wana hali mbaya sana.
Kwa mujibu wa Mohamed Abdikarim, kamanda wa polisi, amesema kuwa, hujuma hiyo ilitokea katika mji wa Wanlaweyn ulio umbali wa kilometa 70 kaskazini mwa Mogadishu. Kadhalika amefafanua kuwa, wahanga wote wa hujuma hiyo ni raia wa kawaida. Mji wa Wanlaweyn unakaribiana na kambi ya kijeshi ya Marekani ambapo askari vamizi wa nchi hiyo huongozea ndege zake zisizo na rubani katika kufanya mashambulizi ya kinyama ndani ya maeneo tofauti ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Genge la kigaidi na ukufurishaji la ash-Shabab limekuwa likidhibiti maeneo mengi ya vijijini ya Somalia tangu mwaka 2011.