Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 1:40 pm

NEWS : WATOTO LAKI NNE NCHINI CONGO DR WAPO KATIKA HATARI YA KUFA NJAA

UNICEF: Watoto laki 4 Kongo DR wapo katika hatari ya kufa njaa

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umesema watoto laki nne wapo katika ncha ya kupoteza maisha kutokana na baada la njaa linalowasakama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika ripoti yake ya jana Ijumaa, UNICEF imesema malaki ya watoto wadogo wanakabiliwa na hali mbaya katika mkoa wa Kasai, katikati mwa nchi na kwamba wanahitaji msaada wa dharura.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema linahitajia takriban dola milioni 88 za Marekani kuwakwamua watoto hao kwenye hatari ya kufa njaa.

UNICEF imesema mapigano kati ya maafisa wa serikali na wapiganaji wa magenge ya waasi yamewaweka watoto hao katika mazingira magumu ya njaa, uchochole na mgogoro mkubwa wa kibinadamu.

Maafisa wa UN nchini Kongo DR

Christophe Boulierac, msemaji wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa amesema watoto wasiopungua 770,000 wanaandamwa na utapiamlo, ambapo laki nne miongoni mwao wanakodolewa macho na kifo kutokana na utapiamlo wa kiwango cha juu walionao.

Amesema kwa ujumla watu milioni 3 na laki nane wanahitaji msaada wa kibinadamu katika mkoa wa Kasai nchini DRC, na kwamba UNICEF inatazamiwa kutoa ripoti yao rasmi leo Jumamosi mjini Kinshasa, pambizoni mwa maafisa wa serikali