- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATANZANIA WAHAMASISHA KUTUMIA KIKOA CHA DOT AFRICA
DODOMA: Watanzania wamehamasishwa kusajili na kutumia kikoa cha dot Africa ili kujivunia uafrika wao,kupunguza gharama za mawasiliano na kujenga uchumi unaotegemea rasilimali ya kikoa katika nchi na bara zima la Afrika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu R. Ntahigiye (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela.
. Wito huo umetolewa leo mjini Dodoma na mtendaji mkuu wa dot Africa LUCKY MASILELA wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kampeni ya matumizi ya dot Africa.
Masilela amesema umuhimu wa kampeni hiyo sio kubeza bali unalengo la kudhihirisha ni jinsi gani Afrika inajenga mhimili muhimu wa mawasiliano katika intaneti kwak uwaunganisha waafrika kwa utambulisho wa kipekee kupitia dot Afrika ili kuimarisha uchumi wan chi zilizopo katika bara hilo.
Washiriki wa kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma walipokutana na waandishi wa habari leo mkoani Dodoma.
Amesema kupitia fursa hiyo watanzania sasa wataweza kuwasiliana,kutoa huduma,kufanya biashara bila ya bughudha yoyote katika mtandao wa intaneti.
Kwa upande wake mhadhiri msaidizi wa kituo cha uratibu wa programu za Microsoft kutoka chuo kikuu cha Dodoma(UDOM)Matogoro Jabhera amesema kama chuo wanajitahidi kuhakikisha lugha ya kiswahili inakuwa na maudhui kwenye intaneti.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dododma Ndg. Jabera Matogolo(wakwanza kulia) akielezea namna ambavyo mtandao wa intaneti unavyosaidia kukuza kiswahili wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma.Kufuatia Umoja wa Afrika(AU)kuridhia maombi ya rajisi ya dot Africa kufanya kampeni ya matumizi ya kikoa cha dot Africa walianisha maeneo matano katika bara hili ya kufanya kampeni kwa niaba ya bara lote la Afrika ambapo kwa Tanzania mbali na shughuli nyingine wanatarajia kupanda mlima Kilimanjaro.