- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WASICHANA 500 NDOA ZA UTOTONI DOM.
DODOMA: Wasichana 500 wa rika kati ya miaka 14 , wamekutwa katika ndoa za utotoni, huku wengine wakiwa hawajui vizuri kusoma na kuandika.
Idadi hiyo imepatikana katika Kata mbili za Segela Kongwa na Bahi, ambapo Taasisi ya Elimu ya watu wazima ilipata idadi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya walimu na maafisa Elimu wa Wilaya ya Bahi na Kongwa Mkufunzi Mkazi wa Elimu ya watu wazima Habibu Muyula alisema hali hiyo inatia hofu sana kwa kuwa ni vijana wadogo sana.
Hata hivyo alisema katika mradi huo ambao unaendeshwa kwa awamu utatumika kuzikomboa Kata ambazo zina watu wa aina hiyo ili kuhakikisha wanajitambua.
Alisema moja ya elimu ambayo wataitoa ni pamoja na kujitambua,kujua haki zao,kujua mazingira,na uraia wao katika sehemu ambayo wanatakiwa wawe.
Alifafanua zaidi kuwa lengo lao ni kuona kila msichana anapata haki yake katika mazingira stahiki,na kupitia mradi huo wa kupinga ukatili wa ndoa za utotoni,unaosimamiwa na Taasisi ya Elimu ya Watu wazima,Sido na Kiwohede wanaamini watafanikiwa.
Alisema idadi hiyo inatakiwa kupungua ikiwezekana kutokomezwa kabisa katika Kata hizo ambazo zitaanza hilo zoezi.
Kwa upande wake mgeni rasmi Gosbert Damaza ambaye aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Mkoa,alisema anawapongeza Taasisi hiyo kwa wanalolifanya huku akiwataka kuongeza bidii katika hilo.
Alisema ni jambo jema na anaamini kupitia mradi huo wa kupinga ndoa za Utotoni watafanikiwa kuwainua wasichana wengi ambao wameathirika na suala hilo.
Alisema kutokana na hilo yeye kana mwakilishi wa Afisa Elimu mkoa anaungana nao katika kuendeleza gurudumu la kupambana na ndoa hizo za utotoni ambazo zimekuwa tatizo sugu.
Alisema watakuwa pamoja kushirikiana kuhakikisha wanafanikiwa kuwakomboa watoto wa kike katika suala zima la Ndoa za utotoni.
Hata hivyo alisema suala hilo linapaswa kupigiwa kelele ili wazazi waache kuozesha watoto wakiwa wadogo badala yake wawapeleke shuleni kwa ajili ya kutimiza ndoto zao za kila siku.