Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 11:49 am

NEWS: WASHTAKIWA KESI YA BILIONEA MSUYU WAHUKUMIWA KUNYONGWA

Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Leo july 23 imewahukumu washtakiwa watano kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite Bilionea Erasto Msuya

Pia mahakama hiyo imemuachia huru mtuhumiwa mmoja kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani.

Msuya aliyekuwa akimiliki vitega uchumi kadhaa ndani na nje ya Arusha, aliuawa kwa kutumia bunduki ya kivita ya SMG, Agosti 7, 2013 katika eneo la Mijohoroni wilayani Hai.