- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANNE WABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUGUSHI RISITI ZA EFD
Dar es salaam: Serekali imewafikisha mahakamani wafanyabiashara wanne na mkulima mmoja katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka tisa ya kughushi risiti za mashine za kieletroniki (EFD) za kampuni mbalimbali hapa nchini
Akiongea mbele ya mahakama kwa niaba ya serekali leo Juni 28, 2018 Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa mbele ya hakimu Augustine Ruizile amewataja washtakiwa hao kuwa ni Cost Nsolo (23) mkazi wa Mbagala, Monica Manase Mnuna (34) mkazi wa Kimara, Sumo Laurent Njige (45) mkazi wa Kimara, Maulid Ally Mchila (38) mkazi wa Kigamboni pamoja na Brian Paul Minja (43) mkulima na mkazi wa Tabata.
Baada ya Msigwa kusomewa mashtaka hayo washtakiwa wote waliyakana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Ruizile alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa hao, kutaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mdhamini atasaini bondi ya Sh 5 milioni. Washtakiwa walikamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa huru.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi july 13, 2018.