- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WANAWAKE WALIOJIUNGA NA KUNDI LA KIGAIDI LA ISIS WAFUNGWA JELA NCHINI IRAN
Wanawake 16 waliokuwa wamejiunga na kundi la magaidi wakufurishaji wa ISIS au Daesh wamehukumiwa vifungo jela nchini Iran.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa Tehran Bw Ja'afari Dolatabadi, wanawake hao walikuwa wameenda nchini Syria kwa lengo la kuunga mkono kundi la kigaidi la ISIS na walikamatwa punde baada ya kurejea Iran.
Akizungumza Jumapili, Dolatabadi amesema wakiwa nchini Syria wanawake hao walipata mafunzo ya kutekeleza mashambulizi ya kigaidi na kwamba wakiwa nchini humo walitekeleza oparesheni kadhaa za kigaidi. Aidha amesema baada ya kuhukumiwa vifungo jela, wanawake hao pia wametakiwa kukabidhi dola 72,000 ambazo walikuwa wamepokea kutoka kundi la ISIS.
Mwendesha Mashtaka wa Tehran ameashiria pia uhasama wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kubaini kuwa: "Serikali ya Marekani inajaribu kupunguza ushawishi wa Iran katika eneo kwa kuunga mkono makundi yanaoupinga mfumo wa Kiislamu."
Ja'afari Dolatabadi ameendelea kuashiria hatua za uhasama wa Marekani dhidi ya Iran na kuzitaja kuwa ni pamoja na kuvuruga mshikamano wa kisiasa nchini, kuhujumu Iran kupitia mitandao ya intaneti na kuchochea uhasama wa kikabila au kikaumu nchini.
Wanawake hao 16 wamefungwa jela huku Mahakama ya Mapinduzi ya Kiislamu Tehran jana ikiendelea kusikiliza kesi za magaidi wa kundi la ISIS ambao walihusika na hujuma za kigaidi mjini Tehran mwezi Juni mwaka 2016 ambapo watu 17 walipoteza maisha. Katika hujuma hizo zilizolenga Bunge la Iran na Haram Takatifu ya Imam Khoemini MA, watu wengine 50 walijeruhiwa.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa mstari wa mbele kupambana na magaidi wa ISIS katika eneo na kufuatia mwaliko rasmi wa serikali za Iraq na Syria, imetuma washauri wake wa kijeshi katika nchi hizo na kuzisaidia katika kuangamiza magaidi wakufurishaji wa ISIS wanaopata himaya ya madola ya kigeni hasa Marekani na Saudi Arabia