Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:48 pm

NEWS: WANAWAKE NCHINI SAUDIA WARUHUSIWA RASMI KUENDESHA MAGARI

Riyadh: Nchi nyingi Duniani ni jambo la kawaida kwa wanamke kuendesha na Kumiliki magari lakini ilikuwa ni tofauti kwa miaka yote kwa wanawake nchini Saud Arabia sasa ni rasmi wameruhusiwa kukaa kwenye usukani, baa ya miongo kadhaa kutopata ruhusa hiyo.

Mabadiliko haya yalitangazwa mwezi Septemba mwaka jana na Saudi Arabia ikatoa leseni za kwanza kwa wanawake mwanzoni mwa mwezi huu.

Ilikuwa nchi pekee iliyobaki duniani ambapo wanawake walikuwa hawaendeshi magari na familia zao zilikuwa zinakodisha dereva kwa ajili ya wanawake.

Hata hivyo, hatua hii imefikiwa wakati kukiwa na Kampeni ya kuwakamata wanaharakati ambao wamekuwa wakipaza sauti wapatiwe haki ya kuendesha magari.

Takriban wanaharakati wa haki za wanawake wanane wanashikiliwa na huenda wakafikishwa mahakamani na kupatiwa kifungo kwa uanaharakati wao, Shirika la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International limeeleza.

Miongoni mwa wanaoshikiliwa ni pamoja na Loujain al-Hathloul, mwanaharakati kinara katika kampeni hiyo.

Amnesty pia imetaka kufanyiwa mabadiliko makubwa nchini Saudi Arabia, ambapo wanawake bado wameendelea kukandamizwa na sheria zinazowapa mamlaka zaidi wanaume.

Kundi hilo la haki za binaadamu limefanya kampeni kwa miaka mingi kuhakikisha wanawake wanaendesha magari.

Wanawake kadhaa walikamatwa mjini Riyadh mwaka 1990 na baadhi walianza kutuma picha za video wakiwa wamekaa nyuma ya usukani mwaka 2008 na kati ya mwaka 2011 na 2014.