- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAUME WATAJWA KUWA KICHOCHEO CHA WANAWAKE KUJIBUA NGOZI.
DODOMA: Baadhi ya wanaume nchini wanatajwa kuwa kichocheo cha wanawake kutumia vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo vimekuwa vikiwapa madahara ya ngozi.
.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Meneja wa Mamlaka ya chakula na dawa Kanda ya kati (TFDA)Dk Englibert Bilashoboka wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili ofisini kwake.
Aidha Dk Bilashoboka amesema kuwa wanawake wengi hujikuta wakitumia vipodozi hivyo kujichubua ngozi zao ili kuwavuti wanaume ambao wamekuwa kichocheo kwa kutamani wanawake wenye rangi nyeupe.
“Wanawake wengine hutunia vipodozi vyenye madhara katika ngozi zao hali wakijua kabisa kuwa vimekatazwa na kujikuta wanapata madhara ,akubwa kiafya na kutumia gharama kubwa katika kujitibu,”amesema.
Pamoja na hayo amesema,licha ya kwamba mamlaka hiyo (TFDA)inafanya juhudi kubwa ya kuielimsha jamii juu ya madhara yatokanayo ya matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu mwitikio bado mdogo.
Katika hatua nyingine meneja mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya kati(TFDA)amesema kuwa, mbali na vipodozi kuchakachuliwa bidhaa nyingine kubwa ambayo imekuwa ikichakachuliwa ni kilevi aina ya mvinyo.
Aidha amefafanua kuwa mamlaka hiyo kwa kushirikiana na raia wema wamebaini kuwepo kwa hali hiyo kutokana na kutumia mfumo wa ufuatiliaji wa bidhaa katika soko.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuwa makini kuangalia taarifa kuhusu muda wa kwisha kwa bidhaa wanazonunua ili kulinda afya zao.
“Kutokana na mfumo wa ukaguzi bora hivi sasa mamlaka hii imefanikiwa kudhibiti Vipodozi bandia ambapo hivi sasa kuna kesi mbili Mahakamani”amesema.
Mbali na hayo ameeleza changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hususan pale wanapofanya kaguzi bidhaa bandia kuwa ni kuingizwa kwa njia za panya au magendo kutokana na mipaka mingi kuwa wazi.