Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 11:54 pm

NEWS: WANANCHI WA KIGOMA UJIJI KUNUFAIKA NA MRADI WA BARABARA ZA LAMI

KIGOMA: Meya wa Manispaa ya Kigoma ujiji Hussein Ruhava leo June 8 amesaini Mkataba wa ujenzi wa Barabara za viwango vya Lami nzito zenye jumla ya kilometa 12 zitakazojengwa ndani ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwenye Jimbo ambalo linaongozwa na Mbunge wa ACT Wazalendo Ndg Zitto Kabwe

Barabara hizo zinajengwa chini ya Ufadhili wa Bank ya dunia kwa Ushirikiano na Bank ya hapa nchini Bank ya NMB .

Barabara zitakazonufaika na Mradi huo ni zile za Maweni - Burega, Ujiji ( ACT Wazalendo Mkoa ) - Kagera ( Mto Luiche ), Mwembetogwa - Kitambwe- Mjini ( Msikiti wa Ijumaa Kigoma ) na Ujenzi- Nazareth, zingine ni Kagashe- Katubuka, Kamata - Simu ( Simu streets kuanzia Muungano Primary- Polisi Mjini)

Akitoa Taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook Mbunge wa Jimbo hilo Zitto Kabwe amewashukuru sana wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa na uvumilivu "Nawashukuru Sana Wananchi wenzangu kwa uvumilivu wenu mkubwa kwani kulikuwa na changamoto nyingi sana katika kuhakikisha mradi huu haupotei. Benki ya Dunia ilikuwa imegoma kabisa kuendelea na mradi mpaka tulipe madeni yaliyotokana na ubadhirifu uliofanywa na Baraza la Madiwani lililokwisha. Nawashukuru sana Benki ya NMB kwa kutuelewa na kutupa facility iliyotatua kero hiyo." alisema Zitto

Aidha Zitto amemshukuru sana waziri wa zamani wa Tamisemi "Namshukuru sana aliyekuwa Waziri wa Nchi TAMISEMI kwa ndg. Simbachawene kwa kutupa msaada mkubwa kipindi tunahangaika kuokoa mradi huu muhimu sana"

Zitto pia amewataka wakandarasi kutokuchelewesha kukamilika kwa mradi huo.