- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Wananchi wa Dodoma wakabiliwa na ukosefu ya vituo vya afya.
Dodoma: Wananchi wa kijiji cha mkoka mkoani Dodoma wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mazingira mazuri kwa ajili ya wamama wajawazito wanao subiri kujifungua pamoja na watoto, hali inayosababisha adha kubwa kwa wamama pamoja na watoto.
Akiongea na muakilishi mkazi wa kijiji cha Mkoka mkoani Dodoma Bw. Thomson Ndule amesema kuwa wanakabiliwa na tatizo la wodi na eneo kwa ajili ya kupimia watoto wanaofikishwa kwa ajili ya kuwajulia maendeleo yao kiafya.
Akielezea tatizo hilo Daktari Festo Mapunda ambaye ni mganga mkuu katika wilaya ya kongwa amesema uchache wa majengo katika vituo vya afya ndiyo chanzo cha kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema katika wilaya ya kongwa vipo vituo vya afya visivyo zidi vinne.