- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Wananchi mkoani Dodoma watakiwa kuwa wazalendo na mji wao
Dodoma: Afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA Dodoma Bw Konradi shio amezungumza na wakazi wa mji Dodoma leo kuwa wanapaswa kuendeleza mji wao kwa kuuthamini na kuulinda mji huo, pia amewataka kuwa wazalendo kwa kuonesha utayari katika kuboresha na kujenga mji wa Dodoma ukiwa ni makao makuu ya nchi.
Akizungumza na muakilishi afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini Sumatra Dodoma bw konradi shio amewataka wanachi mkoani Dodoma kuonesha utayari kwa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuujenga mji wa Dodoma.
Bw shio ameongeza kuwa uzalendo ni jambo la msingi katika maboresho ya mji huo kwani wananchi wasipofanya hivyo zoezi la ujenzi wa makao makuu halitakamilika kwa muda muafaka. Pia amewasihi madereva wote mkoani hapa kuzingatia sheria na taratibu za umiliki na matumizi ya vyombo vya moto.