- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKULIMA WASHAURIWA KUZALISHA MAZAO YENYE UBORA.
Aidha wakishauriwa kuepuka kutumia watu kati wakati wa kuuza mazao yao lengo ikiwa ni kuepusha hasara.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na katibu mkuu ofisi ya makamu wa rais Dkt faustene kamuzora wakati akifungua mkutano wa wadau wa mfumo wa stakabadhi za ghala .
Awali akisoma risala kwenye mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya stakabadhi za Ghala Augustino W. Mbulumi amesema mafanikio yanayopatiakana katika stakabadhi wa ghala hilo ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao,kusaidia kuratibu shughuli hizo, kusaidia kupata taarifa kiurahisi na kuongeza uzalishaji wa mazao pamoja na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.
Aidha wameweza kubainisha changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi,ukosefu wa watumishi na kuishauri serikaoli kuongeza watumishi ili kuwasaidia kufanyakazi kwa urahisi.
Lengo la mkutano huo ni kujadili utekelezaji wa mafunzo,uboreshaji wa huduma za fedha vijijini na manufaa ya soko la bidhaa.