Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 1:36 pm

NEWS: WAKULIMA WAISHAURI SERIKALI KUBORESHA UPATIKANAJI WA PEMBEJEO BORA .

DODOMA: Kufuatia Wizara ya kilimo, mifugo na maji kuwasilisha makadrio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Wadau wa kilimo wameishauri wizara ya kilimo ishirikiane na wizara , Taasisi nyingine na serikali kuboresha mfumo wa taarifa na masoko kiujumla ili kusaidia wakulima kuuza mazao na bidhaa zao katika bei nzuri lengo ikiwa ni kupunguza kwa kiasi kikubwa cha upotevu na mavuno na hasara kwa wakulima.


Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma na mwenyekiti wa jukwaa la wakulima wanawake wilaya ya chamwino (JUWACHA) lililopo chini ya shirika lisilo la kiserikali la Action Aid Janeth Nyamayahasi wakati akitoa maoni ya asasi za kiraia na wakulima kuhusu bajeti ya wizara ya kilimo kwa mwaka 2018/2019.


Aidha Nyamayahasi ameendela kuishauri wizara hiyo kuweka mfumo bora wa bima hususani kwa wakulima wadodo wadogo ili kuhakikisha usalama wa mchakatowa kilimo,wizara kuongeza uwekezaji katika kilimo cha umwangiliaji wenye ufanisi ili kukabiliana na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

''Wizara inahitaji kufanya jitihada mahususi za kuchochea mchakato wa kujumisha masuala ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi katika bajeti kwa kuweka kifungu cha bajeti au kasma mahususi ya mabadiliko ya tabia ya nchi katika bajeti ya Wizara ,''ameongeza kwa kusema mwenyekiti huyo.

Hata hivyo amesema kuboresha upatikanaji wa pembejo bora kwa wakati na gharama nafuu,kuweka vifungashio vya mbolea kwa kiwango kuanzia kilo tano na si kilo 25 na 50 pekee na kuboresha uzalishaji wa mbegu kwa vyanzo vya ndani ili kupunguza upungufu wa aslimia 64 ambazo huagizwa kutoka nje na kuwa na bei ya juu.

''Wizara iboreshe mfumo wa upatikanaji wa taarifa za bajeti zenye uwiano,Wizara iimarishe uratibu ikishirikiana na Wizara ya fedha na Wizara na taasisi nyingine zinazohusika ba uandaaji na uhifadhi wa taarifa,''

Wakati huu huo wizara ya kilimo, mifugo na maji imewasilisha bungeni bajeti yake na kuliomba bunge kulidhia bajeti ya wizara hiyo ya zaidi ya shilingi bilioni 170.2 ambapo ,wabunge wamelalamikia kupunguzwa kwa bajeti ya wizara hiyo wakidai kuwa wakulima nchini wataendelea kudidimizwa.

Naye Waziri wa Kilimo Charles TIizeba amesema Robo tatu ya watanzania wote ni wakulima ambao hutegemea kilimo kama njia pekee ya kujipatia kipato na kukuza uchumi wao.

Pamoja na hayo wakulima kutegemea kilimo lakini pia serikali inategemea kilimo kama njia pekee ya uzalishaji malighafi kwa ajili ya viwanda wakati huu inapojikita kuwa na taifa linalotegemea uchumi wa viwanda.

Licha ya kuwepo kwa changamoto hizo serikali imesema kuwa imedhamiria kufanya mageuzi makubwa kama nchi kwenye sekta ya kilimo.

Kwa mujibu wa kamati ya bunge ya kilimo,mifugo na maji sekta ya kilimo cha umwagiliaji nayo imeendelea kutopewa msukumo wa kutosha na hivyo kutoonesha dhamira ya dhati ya serikali kuinua sekta ya kilimo kupitia umwagiliaji na kuepuka kilimo cha kutegemea mvua