- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA MASOKO.
MLALO TANGA: Imeelezwa kuwa Ili kuboresha sekta ya kilimo Serikali inatakiwa kuongeza idadi ya masoko nchini lengo ikiwa ni kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.
Hayo yamebainishwa leo na wakulima wa kijiji cha KangagaiKata ya Mwagoiwilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wakati wa ziara ya Mbunge wa Mlalo Rashid Shangazi alipotembelea kituo cha habari na mafunzokwa wakulima wa kikundi cha Mwagoi, kituo cha kukusanya maziwa Uwamwa na Mradi wa ufugaji nyuki vyote vikiwa kata ya Mwagoi wilayani Lushoto Mkoani Tanga.
Kaimu mwenyekiti wa kikundi Cha Mwagoi Tatu Kiruwa amesema changamoto kubwa inayowakabili, wanalima mazao lakini masoko yanakuwa shida na kuongeza kuwa pembejeo za kilimo bado ni tatizo kubwa hasa kwa wakulima wadogo wadogo.
Wakizungumzia suala la maziwa wananchi hao wamesema katika kituo cha kupozea maziwa kimewasaidia watu kuweza kuwasomesha watoto wao.
Akijibu Changamoto zinazowakabili wakulima wa kata ya Mwangoi ikiwemo ya Ukosefu wa Majina umeme Mbunge wa jimbo hilo amesema wao kama halmashauri watahakikisha changamoto hizo zinatatuliwa, lengo ni kuwaelekeza wananchi jinsi ya kufunga mashine ziweze kufanya kazi.
Hata hivyo ameendelea kwa kusema Taki la Kupokerea na kupozea maziwa (Tanzu) lenye uwezo wa lita 1500 walilopewa kwa hisani ya Tanga fresh mahitaji bado ni makubwa kwani taki hilo linapokea lita chini yamia tano kwa siku.