- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKULIMA KILIMO CHA ZABIBU KITASAIDIA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA.
Dodoma: Serikali ya chamwino mkoani Dodoma kwa kushirikiana na baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini wamesaini mkataba wa uwekezaji katika ujenzi wa kiwanda cha kusindika zabibu jatika eneo la chinangali 2[two]utakaogharimu zaidi ya shilingi billion 15.
Hayo yamebainishwa na afisa kilimo wilaya ya chamwino, Godfrey Mnyamale leo katika ziara ya kutembelea eneo ambalo litakalojengwa kiwanda cha kusindika zabibu.
Wakulima wa zao la zabibu wamesema wamekuwa wakizalisha kwa hasara kutokana na kukosekana kwa soko la uhakika ambapo wanaamini endapo kutapatikana kwa soko la uhakika litawawezesha kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Joyce Shaidi ambaye ni msimamizi wa mikataba ya sera wa mifuko ya hifadhi ya jamii amesema lengo la kuwekeza kwenye viwanda ni kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa viwanda huku mkurungezi wa halmashauri ya wilaya ya chamwino Athumani Masasi amesema wapo tayari kushirikiana na wawekezaji kataika ujenzi wa viwanda.