Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 10:33 pm

NEWS: WAJUMBE WAMNG'OA MADARAKANI MWENYEKITI WA MTAA.

Dodoma: Wajumbe kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa wa mlimwa kusini kata ya Ipaga mkoani Dodoma wamemuondoa madarakani aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa huo Ismail Sefu kwa madai ya ubadhifu wa fedha za umma na kumteuwa mwenyekiti wa muda Joseph Kalani ambaye kapata kura 115 kati ya wapiga kura 119 ambaye atasimamia shughuli za mtaa huo mpaka pale utakapo fanyika uchanguzi mwingine.

Sefu anatuhumiwa na tuhuma 5 Miongoni mwa tuhuma hizo Zilizotajwa ni

1. kuuza viwanja kiholela kinyume na matakwa ya wananchi

2. kula fedha za ujenzi wa barabara.

Mndeme amesema uteuzi huo umefanyika na wajumbe 6 wanne wakaonesha hawanaimani naye na 2 walionesha wanaimani naye ndipo wakaitisha mkutano wa hazala kwa kushirikiana na wananchi wamemteuwa mwenyekiti wa muda, ambapo uchanguzi huo umefanyika katika ofisi ya serikali ya mtaa ya mlimwa kusini na kusimamiwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme.

Katika uchanguzi huo wananchi waliweza kueleza matatizo na changamoto za mtaaa huo kuwa ni

1.ukosefu wa uwanja wa mpira.

2.ukosefu wa madapo yakumwaga taka.

3. wananchi kudhurumiwa viwanja vyao.


Mndeme amesema mpaka sasa serikali inamipango mizuri ya kuboresha mji na kuleta maendeleo.

baadhi ya mipango ya serikali katika makao makuu ya Tanzania Dodoma ni

1.wametenga hekta 140 maeneo ya Nala kwaajili ya Kujenga uwanja wa mpira.

2. Kutanua huduma za maji.

3.Wametenga hekta 1240 kwa ajili ya kujenga kituo cha afya.

4.kujenga Bandari kavu maeneo ya Ihumwa.

Lakini pia Mndeme amewasisitiza wananchi kufanya kazi kwa bidii kuachana na maneno ya mitaani kikubwa kuepukana na matapeli wanaowadanganya nakuuza viwanja kiholela chamsingi watambue ardhi ya Dodoma inathamani kutoka na serikali kuhamia huku.