- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS :WAISRAELI WAJIUNGA NA WAPALESTINA KATIKA MAANDAMANO DHIDI YA US
Mamia ya Waisraeli wamejiunga na Wapalestina katika maandamano ya kupinga hatua ya kiuhasama ya Marekani ya kuuhamishia ubalozi wake katika mji wa Quds Tukufu, kutoka Tel Aviv.
Katika maandamano hayo ya jana Jumamosi katika mji wa Baitul Muqaddas, waandamanaji hao walisikika wakipiga nara zinazosema. "Jerusalem (Quds) usikate tamaa, tutautamatisha mzingiro."
Kadhalika waandamanaji hao walisikika wakimtaka Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu ajiuzulu, wakiimtaja kama nembo ya uhasama, chuki na taharuki.
Baadhi ya waandamanaji walisikika wakisema "Jiuzulu Netanyahu", "Amani ina thamani zadi yako", "Usiiteketeze moto Jerusalem", na "Hauna haya hata kidogo, hakuna utakatifu kwa kuukaliwa kwa mabavu mji."
Juzi baada ya Sala ya Ijumaa, maelfu ya Waislamu katika nchi za Uturuki, Indonesia na Jordan walifanya maandamano wakipiga nara za kulaani chokochoko hizo za Marekani huku wakiwa wamebeba bendera ya Palestina.
Licha ya upinzani kutoka kila kona ya dunia, lakini Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kuwa, siku chache zijazo serikali ya Washington itafungua ubalozi wake katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel