Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:19 am

News: Wahamiaji Raia wa Afrika wauzwa utumwani Libya.

Afrika: Raia wa Afrika kwanaojaribu kuvuka na kuelekea barani Ulaya, wamekuwa wakiuzwa na watekaji wao na kuuzwa katika “soko la utumwa” nchini Libya.

Taarifa hizo zimetolewa na shirika la kuwahudumia wahamiaji duniani International Organization for Migration (IOM) ambapo waadhirika wa biashara ya utumwa wameliambia shirika hilo kuwa, baada ya kuzuiliwa na walanguzi wa biashara ya watu au makundi ya wapiganaji, wanapelekwa hadi kwenye viwanja vya mji au kwenye maeneo ya kuegeshea magari na kuuzwa.

Kiongozi mkuu w shirika hilo amesema kuwa wahamiaji walio na ujuzi kama vile upakaji rangi au ukulima, wanauzwa kwa bei ya juu, kitendo ambacho kimelaaniwa na umoja wa mataifa na kutaka hatua za haraka zichukuliwe kukomesha matendo ya kutisha dhidi ya wahamiaji .

Libya imekuwa katika ghasia tangu mwaka 2011 pale wanajeshi wa shirika la kujihami la mataifa ya magharibi-NATO yalipomuondoa madarakani Rais wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.