- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAFUNGWA ATOA KILIO CHAO MBELE YA MBUNGE
MNG'ARO TANGA: Wafungwa wa gereza la kilimo Mng’aro MkoaniTanga wameomba kuwepo na vitabu maalumu magerezaniambavyo vitawasaidia kujua haki zaopindi wawapo kifungoni.
Akizungumza katika ziara ya Mbunge wa Jimbo la Mlalo Rashid Abdallah Shangazi leo alipowatembelea gerezani hapo moja ya Wafungwa Riziki Kishita NO/6.2018 amesema kuwa ukosefu wa Sheria zinazoonyesha haki za wafungwa magerezani hupelekea wengi wao kutumikia kifungo bila kujua haki zao za msingi.
Mbali na hayo amesema ukosefu wa tv, radio gerezani kwao ni moja ya changamoto kubwa inayowakabili hali inayopelekea kutopata haki yao ya kupata taarifa.
Mkuu wa gereza hilo Ally Mgaya amesema kutokujua haki za mfungwa ni mfungwa mwenyewe na kuahidi kuwa kuanzia sasa wataandaa utaratibu wakubandika karatasi sehemu mbalimbali za gereza hilo ili ziweze kuwasaidi baadhi ya wafungwa kuweza kutambua haki zao na kuongeza kuwa ukosefu wa sarekwa wafungwa hupelekea kuvalianana askari.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo mbunge huyo ameahidi kupeleka Tv ambayo itawasaidia kupata taarifa ambayo ni haki ya kila raia.