Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 4:51 pm

News: Wadaiwa sugu wapewa siku 14 na Tanesco Kulipa madeni yao

Dar es salaam; shiririka la umeme Tanzania [Tanesco] limetoa siku 14 kwa wadaiwa sugu kuhakikisha wanalipa madeni yao yote vinginevyo hatua za kukatiwa zitafuatia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo alhamis ofisini kwake, kaimu mkurungezi wa shirika hilo, Tito Mwinuka amesema mpaka sasa wanadai billioni 275. kutoka kwa wateja wao, kama utakumbuka hivi karibuni TANESCO Imekaririwa ikisema kuwa itaikatia umeme (ZECO) ambalo ni shirika la umeme la serekali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kushindwa kulipa deni ambalo Tanesco wanaidai Toka zamani Serekali hiyo.

Ameongeza kwa kusema kuwa notisi hiyo ni kwa wateja wote wakubwa na wadogo kama hataweza kulipa deni atakatiwa umeme ikiwamo shirika la umeme zanzibar[zeco] akasisitiza tena. kwa wakati wote TANESCO imekuwa ikilalamika kuwa inaendesha shirika hilo kwa hasara ambayo kimsingi ni kwa sababu ya wadaiwa sugu na pia kuwepo na madeni mengi kutoka kwenye kampuni ambazo zinaiuzia umeme TANESCO Kwa gharama kubwa ya capacity charge.