Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 9:37 pm

NEWS: WACHINA 19 WABURUZWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YAUHUJUMU UCHUMI

Dar es Salaam: Wachina 19 na watanzania 6, wamefikïshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

Wakili wa Serekali Patrick Mwita amesoma hati ya Mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu, Haruma Shaidi na kueleza mahakama kuwa Mnamo June mosi 2017 na mei

18, 2018 washtakiwa hao walitenda kosa chini ya sheria ya watu ambao siyo raia wa Tanzania kwa kutoa taarifa za uongo kwa lengo la kupata kibali cha kufanya kazi nchini. Katika shtaka la pili inadaiwa, siku na mahali hapo hapo, washtakiwa wote kwa makusudi huku wakijua kuwa ni kosa, walitoa taarifa za uongo kwa Kamishna wa kazi kwa lengo la kupata vibali vya kufanyia kazi.

Washtakiwa hao wanashtakiwa chini ya vifungu vya sheria ya uhamiaji, chini ya sheria ya watu ambao siyo raia wa Tanzania na uhujumu uchumi.

Katika shtaka la tatu, mshtakiwa Bo Song anadaiwa kuwa alijihusisha na kazi nchini bila ya kuwa na pasi ya kuishi nchini. Pia washtakiwa wote kinyume na sheria ya uhujumu uchumi wanadaiwa kuwa walijihusisha na makosa ya kiudanganyifu kwa kuonyesha kwamba walikuwa na vibali vya kuishi nchini Tanzania kutoka idara ya Uhamiaji na vibali vya kufanya kazi kutoka kwa Kamishna wa kazi nchini huku wakijua kuwa siyo kweli Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana dhidi ya washtakiwa kwa ajili ya maslahi ya nchi na washtakiwa. Wakili wa utetezi Peter Kibatala alipinga hati hiyo na kudai hatua hiyo ya DPP haizuii mahakama kuangalia na kutoa uamuzi.

Aidha amedai kuwa, hati hiyo haioneshi ni jinsi gani maslahi ya nchi wala watuhumiwa yatakavyoathiriwa. Wakili wa serikali, Mwita amepinga hoja hizo na kudai, kwa mujibu wa sheria ya kesi za uhujumu uchumi, DPP akiweka hati mahakama haina mamlaka ya kuhoji hicho kibali . Baada ya mabishano ya kisheria, Hakimu Shaidi amesema atatoa uamuzi dhidi ya washtakiwa kama wapate dhamana ama la Juni 14, mwaka huu.