- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: wabunge nchini korea kusini wapiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais Park
Soul: Wabunge nchini Korea Kusini wamepiga kura kumuondoa madarakani Rais Park Geun-hye.
Hoja hiyo imepitishwa na wabunge 234 dhidi ya 56.
Maelfu ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakitaka Bi Park aondolewe madarakani.
Hatua hiyo itamlazimisha Bi Park kung'atuka kwa muda huku Mahakama ya Kikatiba ikiamua iwapo ataondolewa kabisa kutoka wadhifa huo wa urais.
Suala kuu limekuwa ni uhusiano kati ya Bi Park na msiri wake mkuu Choi Soon-sil, ambaye anadaiwa kutumia uhusiano huo kujizolea ushawishi nchini
Viongozi wa mashtaka wanasema Bi Park alikuwa na "mchango mkubwa" katika visa kadha vya ufisadi, tuhuma ambazo amezikanusha.
Aidha, alikataa wito wa kumtaka ajiuzulu akisema uamuzi huo aliuachia bunge.