Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:07 pm

News: UN imesema kuwa haitafumbia macho matendo yanayo fanywa na vikosi vya kulinda amani Vya umoja wa Mataifa

New York: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Gutteres ametoa mapendekezo kadhaa yenye lengo la kupambana na unyanyasaji wa kijinsia uliofanywa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kokote Duniani kwa wakazi wa maeneo wanakofanyia kazi.

bwana Guterres anasema malipo kwa ajili ya nchi ambazo hupeleka askari wa kulinda amani zishikiliwe iwapo uchunguzi hautafanyika kwa ufanisi.

Chini ya sheria ya Umoja wa Mataifa, nchi zinazochangia walinda Amani zinawajibika kuwawajibisha askari wake.

Bwana Guterres anasema ikiwa fedha hiyo inaweza kwenda katika mfuko wa waathirika; amependekeza pia kuteua mawakili maalum kusaidia walioathirika.

Aliongeza kwa kusema kuwa bendera ya Umoja wa Mataifa haitatumika tena kufunika uovu unaofanywa na vikosi vya walinda usalama