Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 2:02 am

News: Uhusiano kati ya Urusi na Marekani wazorota toka kuingia kwa Trump Madarakani

Moscow: Tatizo la kutoaminiana kati ya nchi ya Urusi na Marekani yapelekea kuzorotesha Mahusiano baina yao,Jana Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov ameitisha press conference ambapo amekiri kwamba uhusiano kati ya Moscow na Marekani umedorora sana.

jana hiyo Bw Lavrov amekutana na mwenzake waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson, bwana Lavrov amesema Urusi ilikua tayari kwa mazungumzo.

Waziri huyo amesema dunia itakuwa mahali salama ikiwa pande zote zitashirikiana na kuwa na sauti moja .


Na katika Umoja wa Mataifa, Urusi ilipiga kura ya turufu dhidi ya pendekezo kutaka Syria ishirikiane na uchunguzi kuhusu shambulio la silaha za kemikali.

Pendekezo hilo liliwasilishwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa.

Naibu balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vladimir Safronkov amesema pendekezo hilo linahalalisha shambulio la Marekani katika kambi ya wanahewa wa Syria wiki jana.