Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 7:42 pm

NEWS : UGANDA YAITAKA UN KUONGEZA UFADHILI KWA AJILI YA WAKIMBIZI

Serikali ya Uganda imeutaka Umoja wa Mataifa uongeze msaada na ufadhili wake kwa ajili ya makumi ya maelfu ya wakimbizi walioko nchini humo.

Spika Rebecca Kadaga aliyasema hayo jana katika mazungumzo na maafisa wa taasisi kadhaa za Umoja wa Mataifa, walioitembelea nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kutathmini hali ya wakimbizi hao.

Maafisa hao wakiwemo wa Mpango wa Chakula Duniai WFP, Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa kadhalika walikutana na kufanya mazungumzo na Rais Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebbe hapo jana, na pande mbili hizo zilijadili hali ya wakimbizi hao.

Mwezi jana, Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu liliripoti kuwa, wimbi kubwa la wakimbizi nchini Uganda limesababisha msongamano mkubwa katika hospitali na katika kambi za wakimbizi zilizoko nchini Uganda.

Aghalabu ya wakimbizi walioko Uganda ni raia wa DRC waliokimbia vita

Kwa mujibu wa shirika hilo, zaidi ya wakimbizi 40 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo miongoni mwa 70 elfu waliowasili nchini Uganda tangu mwanzoni mwa mwaka, wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu katika kambi hizo.

Idara ya Wakimbizi iliyoko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda na UNHCR zinakadiria kuwa, nchi hiyo itakuwa na wakimbizi zaidi ya milioni 1.8 kufikia mwishoni mwa mwaka huu, kutoka milioni 1.4 mwishoni mwa mwaka jana 201