Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 1:30 pm

NEWS: UBALOZI MPYA WA MAREKANI KUFUNGULIWA LEO JERUSALEM NCHINI ISRAEL

Jerusalem: Marekani inatarajiwa leo Mei 14, 2018 kuandika historia nyingine ya kufungua ubalozi wake mpya mjini Jerusalem nchini Israel hatua ambayo imesifiwa na Israel yenyewe na kulaaniwa vikali na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa hii leo.

jengo jipya la ubalozi wa marekani

Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner.

Kando na Ivanka Trump na Jared Kushner ambao wote ni washauri wakuu kwenye Ikulu ya White House, Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan watakuwa kwenye sherehe hiyo.

Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner.

Muungano wa Ulaya umepinga vikali kuhamishwa kwa ubalzo huo na mabalozi wengine wa nchi za EU hawatahudhuria sherehe hiyo.


Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mkuu wa badae.

Israel ilichukua udhibiti wa eneo la Jurusalem mashariki mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inahutaja mji huo kuwa wake na usiogawanwa

Hatua hiyo ya Trump ya mwaka uliopita ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilivunja msimamo wa wastani wa Marekani kwa suala la mji huo na kwenda kinyume na misimamo ya nchi zingine duniani.

maandamano ya wapalestina

Rais Trump anatarajiwa kuhutubia wale amboa watahudhuria sherehe hiyo kwa njia ya video.

Hata hivyo wanadiplomasia kadhaa wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo waakilishi kutoka Hungary, Romania na Jamhuri ya Czech ambayo ilizuia taarifa ya pamoja ya EU kuhusu suala hilo.

Marais wa Guatemala na Paraguay pia nao wanatarajiwa kuhudhuria; nchi hizo zote mbili ziliamua kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem baada ya Trump kutoa tangazo hilo.

Tangu mwisho wa mwezi Machi zaidi ya wapalestina 40 wameuawa na wanajeshi wa Israel wakati wa maandamano ya mpakani.

Mku wa shriika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ameilaumu Isreal kwa kutumia nguvu nyingi.

Hali ya mji wa Jerusalem ndiyo chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina.

Tangu mwaka 1967 Israel ilijenga makao mengine kwa karibu wayahudi 200,000 huko Jerusalem mashariki. Makao hayo yanatajwa kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa, licha ya Israel kupinga hilo.