- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TUZO MAARUFU YA NOBEL YAHAIRISHWA KUTOLEWA KWA KASHFA YA NGONO
Sweeden: Taarifa zinasema kuwa Hakutakuwa na Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka huu. Tangazo lilitolewa Ijumaa asubhi wiki hii, huko Stockholm, na Chuo cha Sweden. Taasisi inayotoa tuzo ya nobel ya fasihi imesema kuwa hapatakuwepo kwa tuzo hiyo mwaka huu.
Taasisi hii ilifadhaika kwa miezi kadhaa, kufuatia kufichuliwa kwa visa vya unyanyasaji wa kijinsia na matumizi mabaya ya kifedha katika taasisi hiyo.
Taasisi hiyo ya Sweden imekuwa kwenye mzozo mkali kutokana na namna wanavyoshughulikia shutuma dhidi ya mume wa mfanyakazi wa taasisi hiyo
Taasisi imesema itatangaza mshindi wa mwaka 2018 na mshindi wa mwaka 2019 mwakani.
Uamuzi huu wa kuahirisha Tuzo ya Nobel ya Fasihi, ambayo haijawahi kuchukuliwa tangu mwaka 1949, ni matokeo ya yanayoikabili taasisi hiyo inayotoa tuzo ya nobel ya fasihi.
Mgawanyiko ulianza kujitokeza mwezi Novemba mwaka jana baada ya mpiga picha raia wa Ufaransa Jean-Claude Arnault aliyekuwa akifanya kazi ya kuongoza mradi wa maswala ya tamaduni uliokuwa ukifadhiliwa na shule ya Sweden, alikuwa akishutumiwa kuwadhalilisha kingono wanawake 18.
Jean-Claude Arnault
Wanawake kadhaa kati yao waliripoti kuwa vitendo hivyo vilifanyika kwenye maeneo yanayomilikiwa na shule hiyo. Hata hivyo Jean-Claude Arnault amekana shutuma hizo.