Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:33 pm

NEWS: TRUMP ASITISHA MPANGO WA KUWATENGANISHA WATOTO NA WAZAZI WAO

Washington: Rais wa Marekani Bw. Donald Trump amebadili msimamo wake siku ya jana Jumatano na kutia saini amri ya utendaji (executive order) inayositisha hatua ya kuzitenganisha familia na watoto wao wanapoingia Marekani kinyume cha sheria kwenye mpaka na Marekani na Mexico. Hata hivyo amesisitiza kwamba amri hiyo haitobadili sera yake ya kutowastahmilia wahamiaji wanaojaribu kuingia Marekani kinyume cha Sheria.Image result for trump withdraws separation

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuna mambo kadhaa yaliyomsababisha kuchukua hatua hiyo kwanza inabidi kutaja hapa kwamba Trump tangu alipochukua madaraka na hata kabla hapendi kubadili misimamo au hatua anazochukua.

Pamoja na kulegeza msimamo huo kutokana na kulalamikiwa kwa sera hiyo ndani nan je ya taifa hilo, Trump amesisitiza kwamba bado ataendelea kuilinda mipaka yake.

Rais Trump ambaye tangu kuingia kwake madarakani alionekana kuhitaji sheria kali zaidi ya kukomesha suala la uhamiaji haramu, amejikuta matatani, safari na hasa baada ya picha zenye mguso za watoto waliotenganishwa na wazazi wao katika mpaka wa Marekani na Mexico kuanza kusambaa na kuleta mshituko mkubwa kwa raia wa Marekani.

wachambuzi wanasema mabadiliko ya Jumatano huwenda kwanza yanatokana na mkewe Melania Trump ambaye mapema wiki hii kupitia msemaji wake alisema haungi mkono zoezi la kuwatenganisha watoto na wazazi wao, baada ya matamshi ya wake watatu wa marais wa zamani wa Marekani kusema matamshi kama hayo akiwemo Michelle Obama, Hillary Clinton na Laura Bush.

Pia kuna kilio kikubwa cha kisiasa kutoka kwa wahafidhina na viongozi wa makanisa wanaomuunga mkono mbali na ukosowaji mkali kutoka kwa wa-Democrats na wa-Republican kwa ujumla na viongozi wa kigeni pamoja na Papa Francis