Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 5:50 pm

News: Trump ashida tunzo ya kiongonzi mwenye ushawishi mkubwa Duniani

Ufarance: Shirika la Habari kubwa Duniani la AFP limemtangaza Rais wa Marekani Bwana Donald Trump kuwa ndiye kiongonzi mwenye ushawishi mkubwa duniani, shirika hilo lenye makao yake makuu Paris nchini Ufarance limemuweka Trump Juu ya viongozi wengine Duniani kama Rais wa Urusi Bwana Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan Rais wa Uturuki kama kiongozi mmenye ushawishi zaidi Duniani

Chombo cha AFP kina waandishi wa habari karibu duniani kote, na kinajitahidi kufanya kazi katika lugha zote na waandishi wa shirika hilo walipiga kura kumchagua kiongoz mwenye ushawishi zaidi Duniani na kura hiyo kuangukia kwa Trump na kukaa juu ya Rais wa Urusi na Uturuki ambao walishika nafasi ya pili na ya tatu

AFP waandishi wake wa habari walichagua kutoka orodha ya watu 30 kwa maana ya wahariri wakuu kutoka sehemu mbalimbali za shirika hilo. Kama utakumbuka Trump toka kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama chake cha Republican kutafuta muakilishi atakaye kiwakilisha chama chao amekuwa maarufu mpaka anachaguliwa kupata uraisi wa marekani. Katika mchakato wa kumpata mtu mwenye ushawishi zaidi Duniani kwa mwaka 2016, AFP kiliwatumia zaidi ya waandishi 300 walipata nafasi ya kupendekeza.

Hii ndio list ya watu wenye ushawishi mkubwa duniani

1.Donald Trump

2.Vladimir Putin

3-Recep Tayyip Erdogan

4-Hillary Clinton

5-Nigel Farage

6-Bashar al-Assad

7-Barack Obama

8-Pope Francis

9-Bob Dylan

10-Michelle Obama