Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 11:40 am

NEWS: TRUMP AJICHANGANYA KAULI ZAKE DHIDI YA URUSI

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye amekuwa akikosolewa vikali, baada ya matamshi yake ya kuitetea Urusi kuwa haikuingilia uchaguzi wa mwaka 2016, amesema hakueleweka vema.

Trump amesema ana imani kubwa na kitengo cha Inteljensia ncnini Marekani ambacho maafisa wake wamekuwa wakisema Urusi iliingilia Uchaguzi huo.

Nina imani kubwa na nawaunga mkono maafisa wetu wa Inteljensia, na nimekuwa nikisema kuwa, hatua ya Urusi haikuwa na atthari yoyote kwa matokeo ya Uchaguzi. Kama nilivyosema, acha nirudie kuwa, nakubaliana na maafisa wa Intejesnia kuwa Urusi iliingia Uchaguzi wa mwaka 2016.

Hata hivyo Kwa upande wake Mark Warner, Seneta kutoka chama cha upinzani nchini Marekani cha Democratic ameweka wazi kwamba hana imani na kauli za kiongozi huyo.

''...Sikubaliani na kauli alizotoa Rais leo. Kama angetaka kutoa kauli hizo, angepaswa kuwa na uwezo wa kufanya hivyo mbele ya Vladmir Putin. Huyu ni Rais ambaye alionesha udhaifu mbele ya kiongozi wa Urusi, alionesha udhaifu mbele ya dunia nzima...'' Alisema Seneta Warne

Urusi imekuwa ikisema hakuingilia Uchaguzi huo wakati huu maafisa wa Iteljesnia wa Marekani wakiendelea na uchunguzi.