- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: TRA YAOMBA RADHI SAKATA LA SERENGETI BOYS KUSIMAMISHA BASI LAO
Dar es salaam: Tukio la Timu ya Taifa ya vijana kwa mpira wa miguu maarufu kama seregeti boys Kusimamishwa na Shirika la ukusanyaji mapato Tanzania TRA ili kulipa kodi lilizua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii sasa leo kupitia Power Break fast cha Clouds fm Msemaji wa TRA Leo ameanza kwa kuomba radhi, "tunaomba radhi kwa makamu wa Rais mama Samia Suluh Hassan na Watanzania wote kwa Ujumla pia na wadau wa mpira kwa tukio la Timu ya Taifa ya Vijana ya Serengeti Boys kwa Kulizuia Bus lilobeba wachezaji wa timu ya Taifa vijana,
alisema kuwa " wale wamebeba bendera ya Nchi sasa Huwa kuna njia tunazitumia katika kukamata mali za mdaiwa lakini si kwa utaratibu ule, kwahiyo kunahatua za kitawala tunazichukua dhidi ya kitendo hicho.
Pia aliye kuwa Waziri wa Sana, Utamaduni na Michezo na Mbuge wa Mtama Mh. Nape Nnauye amelaani vikali tukio hili kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa Tukio hili la serengeti Boys na TRA halikubaliki na halivumiliki si sawa, Nape akahoji ukusanyaji gani wa kodi huu, ujumbe gani wanampelekea makamu wa Rais alihoji Nape.