Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 9:52 am

NEWS: TLS YAJINASIBU KUMTIBU LISSU KWA ZAIDI YA MILIONI 130

Dar es salaam: Chama cha mawakili Tanganyika TLS kimesema kuwa kimefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh.138 mil za kugharamia kumtibu Rais wa chama hicho Tundu Lissu ambaye yupo nchini Ubilgiji kwa matibabu baada ya kupewa rufaa kutoka kwa madaktari wa hospitali ya Nairobi nchini kenya alikokuwa anapatiwa matibabu.

Akiongea kwa niaba ya TLS Makamu mwenyekiti wa chama hicho Bw. Godwin Ngwilima amesema kuwa kiasi hicho wamekipata kutoka kwa wadau mbali mbali waliopo ndani na nje ya Tanzania wakiwemo wanachama wa chama hicho.

Godwin Ngwilima akitoa ufafnuzi

Ngwilima ametoa ufafanuzi juu ya matumizi ya pesa hizo kuwa ni mapoja na kugharamia kulipia matibabu ya mbunge huyo katika hospitali ya Nairobi na kugharamia VISA kwa watu watatu waliosafiri nae kwenda nchini Ubelgiji.

Ngwilima ametoa shukrani kwa niaba ya chama hicho kwa watu na wadau wote waliojitokeza kumchangia pesa za matibabu mbunge huyo.

Lissu alishambuliwa na zaidi ya Risasi 30 mnamo september 7 mwaka jana nyumbani kwake Area D mjini Dodoma, nakupelekwa kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Mkoani Dodoma saa chache kabla ya kusafirishwa kwa matibabu zaidi katika Hospitali ya nairobi nchini kenya ambapo alitibiwa kwa miezi mitatu na baadae kupelekwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi mapaka muda huu.