- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TANZANIA YALIPA DENI LAKE LA SHILING TRILIONI 6
Serekali ya Tanzania imesema kuwa hadi kufikia mwezi Machi 2020 imefanikiwa kulipa deni lake lote lililoiva la Shilingi Trilioni 6.19 ambapo Deni la ndani ni shilingi 4.06 ukijumlisha na Riba.
Taarifa hiyo imetolewa leo mei 15, 2020 Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango huku akisema wizara inaendelea kusimamia Deni la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada Sura 134. Amesema kipaumbele ni kukopa kutoka kwenye vyanzo vyenye masharti nafuu na fedha zinazopatikana kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo, hususan miradi inayochochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi na maendeleo ya watu.
Waziri huyo amesema, wizara inaendelea kuhakikisha kuwa, madeni yote yanayoiva yanalipwa kwa wakati.
“Hadi kufikia mwezi Machi 2020, Serikali ilifanikiwa kulipa deni lake lote lililoiva lenye thamani ya Sh.6.19 trilioni. Kati ya kiasi hicho, deni la ndani ni Sh.4.06 trilioni ikijumuisha riba Sh1.08 trilioni na mtaji Sh.2.98 trilioni,” amesema Dk. Mpango
“Aidha, deni la nje ni Sh.2.13 trilioni ikijumuisha riba ya Sh.636.75 bilioni na mtaji Sh1.49 trilioni,” amesema
Dk. Mpango amesema kwa mwaka 2020/21, wizara itaandaa na kutekeleza mikakati itakayowezesha Serikali kukopa katika soko la fedha la ndani na nje bila kuathiri uhimilivu wa deni la Serikali, Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada Sura 134 na vigezo vya viashiria hatarishi vya madeni yaliyotokana na dhamana za Serikali.