- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAKUKURU WAWAFIKISHA KORTIN MAAFISA WA TUME YA UCHAGUZI MKUU
Maofisa wa halmashauri za wilaya nchini waliosimamia Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015 wameanza kuchunguzwa kwa matumizi mabaya ya fedha.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema baadhi yao wamekwisha kufunguliwa mashitaka wakituhumiwa kuandaa nyaraka za uongo kuficha upotevu wa mamilioni ya shilingi. Miongoni mwao ni aliyekuwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Hassan Mkwizu, anayeshitakiwa kwa makosa ya kughushi nyaraka na kufuja fedha za umma. Mkwizu na Mhasibu Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Mustafa Haji na Mtunza Kumbukumbu, Monica Mkasa wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanga. Mwendesha Mashitaka kutoka Takukuru, Suzan Kimaro, amesoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Mariam Lusewa.
Kwenye hati ya mashitaka, kosa la kwanza linamkabili mshitakiwa wa pili, Mkwizu, anayedaiwa kuwa Oktoba 22, 2015 akiwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika halmashauri hiyo, alighushi nyaraka zenye majina ya watu 220 akidai kuwa walikuwa ni walinzi. Pia anadaiwa kuandaa nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya mwajiri na kuonyesha kuwa walinzi hao walilipwa posho ya jumla ya Sh. milioni 11 kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu wakati akijua si kweli. Katika kosa la tatu, mshitakiwa huyo anadaiwa kufuja Sh. milioni 11 ambazo ni fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga. Mtuhumiwa alikana mashitaka yote. Shitaka la nne linawakabili washitakiwa Haji na Mkasa wanaodaiwa kumsaidia Mkwizu kutenda kosa kinyume cha Kifungu cha 30 cha Sheria ya Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007. Washitakiwa wote walikana mashitaka hayo na wako nje kwa dhamana. Kesi hiyo itatajwa Julai 19, mwaka huu. Takukuru pia imemfikisha mahakamani mfanyabiashara Abdallah Majungu, akishitakiwa kwa kosa la kumsaidia Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Mkwizu, kutenda kosa lililomwezesha kujipatia Sh. milioni 12.4. Imedaiwa kuwa fedha hizo zilitolewa na