- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: TAKUKURU jamii bado haina mwelekeo kuhusu utoaji wa taarifa vitendo vya rushwa.
Dodoma: TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Dodoma (TAKUKURU) imesema kuwa rushwa bado ni tishio kwa baadhi ya taasisi na kwamba ni kichocheo cha kupunguza maendeleo nchini.
Hayo yamebainishwa mapema leo na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Bi.Emma Kuhanga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya taarifa zinazohusu utendaji wa madawati ya uchunguzi ,uchambuzi wa mifumo na elimu kwa umma.
Mbali na hayo Kuhanga amesema kuwa taarifa zilizopokelewa na taasisi hiyo kuhusu dawati la uchunguzi na mashtaka zinaonyesha kuwa mapambano dhidi ya rushwa yanahitaji mchango mkubwa kutoka kwa wana jamii.
Hata hivyo amesema jamii bado haina uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya rushwa pamoja na kuwa taasisi hiyo inatoa elimu na kwamba ni wajibu wa jamii nzima kuungana na kuipinga rushwa.
Vilevile amesema ili kuboresha huduma kwa jamii ni lazima taratibu za mawasiliano ya kiutumishi yaboreshwe na kuzingatiwa kwa kupitia njia rasmi ya maandishi .
Bi Ema amesema kuwa TAKUKURU imebaini kuwa kamati za maji za miradi ya vijiji pamoja na kuwa na jukumu la kusimamia miradi hiyo ,bado haitekelezi ipasavyo ambapo kamati hizo hujikuta zikitumia vibaya mapato ya maji.
Kutokana na hayo TAKUKURU imetoa ushauri kwa jamii kuwachagua wajumbe makini wa kamati za maji ambapo watatakiwa kuzingatia taratibu na kanuni ili kufanikisha utendaji wao.