Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:39 pm

News: Taarifa za kupinduliwa kwa Rais wa Rwanda Paul KAGAME

Dar es salaam: Katika hali isiyo ya kawaida Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, ametangaza kuunda serikali yake licha ya kuwepo utawala uliopo madarakani kwa sasa nchini Rwanda, lakini itakayokuwa ikifanya kazi nje ya nchi.

Thomas Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.

Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.

Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.