- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: TAARIFA ZA KUKAMATWA KWA RAIS WA KOREA KUSINI BI PARK
Seoul: Rais aliye ondolewa madarakani nchini korea kusini kwa kura ya kutokuwa na imani naye ( impeachment) Park Geun-hye amekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na tuhuma za rushwa, Park mwenye umri wa miaka 65, alisafirishwa kwa gari hadi kwenye kituo cha kuwazuilia watuhumiwa wa uhalifu kusini mwa Seoul baada ya mahakama kuidhinisha kukamatwa kwake.
Bi Park anatuhumiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni kubwakubwa. Bi Park amekanusha madai hayo.
Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14.
Waendeshaji mashtaka walisema Jumatatu kwamba "wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata".
Walisema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta huenda ungeharibiwa iwapo Bi Park hangekamatwa.
Bi Choi amefunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa na tayari kesi dhidi yake imeanza.
Bi Park ndiye rais wa tatu wa zamani Korea Kusini kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika uhalifu, shirika la habari la Yonhap limeripoti.
Mahakama ya Seoul ilitoa kibali cha kukamatwa na kuzuiliwa kwa Bi Park anapoendelea kuchunguzwa kuhusu ulaji rushwa, kutumia vibaya mamlaka, kutumia mamlaka yake kushinikiza watu na kuvujisha siri za serikali.
Uamuzi wa mahakama ulitolewa baada ya kikao cha mahakama kilichodumu saa tisa Alhamisi na Bi Park alihudhuria kikao hicho.