Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 8:23 pm

News: Taarifa ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa kamati ya Viwanda na Biashara

Dodoma: Aliye kuwa Mwenyekiti wa kamati ya viwanda, biashara na mazingira ya bunge ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Igunga mkaoni Tabora Dkt Dalaly Peter Kafumu ametangaza kujiuzulu kwa nafasi hio.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za idala ya habari Bungeni mjini Dodoma Kafumu amesema ametangaza kujiuzulu uwenyekiti huo kutokana na kuongezeka kwa majukumu katika utendaji wa kazi ambayo ni moja ya sababu ambayo inamfanya ashindwe kulihudumia na kujua matatizo ya wananchi wa jimbo lake, Ushirikiano hafifu Miongoni mwa wabunge na kukosa nafasi ya kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani jimboni kwake.

''Bado kuna wabunge wengi wazuri wanauwezo wakafanya kazi hiyo mimi ni mtaalamu wa madini au jiolojia na uwezoefu serikalini kwa miaka 33 kwahiyo naamini watu wengi wanauwezo wakutoa mchango wao kwenye nafasi hiyo''. alisema Kafumu.