- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAARIFA YA KINA YA AJALI ILIYOUWA WATU 20 MBEYA
Takriban watu 20 wamepoteza maisha na wengine 48 kujeruhiwa baada ya ajali ya barabarani iliyohusisha zaidi ya magari matatu mkoani Mbeya, kanda ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania, Ajali hiyo ilitokea katika mteremko wa Iwambi mkoani Mbeya.
chanzo : Ajali hiyo ilitokea baada ya lori lililokuwa limebeba kontena lenye shehena ya mzigo, lilikuwa linatokea Mbeya Mjini kwenda Tunduma kugongana na mabasi madogo ya abiria matatu, ambapo moja lililaliwa na lori hilo lenye kontena baada ya kugongwa na kutumbukia mtoni katika eneo la Iwambi, Mkoani Mbeya.
Mabasi hayo madogo ya kuwabeba abiria maarufu kama Daladala ambayo yalihusika kwenye ajali hiyo hufanya safari zake kati ya Mwanjelwa na Mbalizi.
Miongoni mwa waliofariki dunia ni wanaume 10 na wanawake 10 akiwemo mtoto mmoja.
Hii ni ajali ya tatu kutokea Mbeya katika kipindi kifupi ambapo katika ajali hizo idadi ya Watanzania waliopoteza maisha imefikia 40.
Mnamo 14 Juni, watu 13 wakiwemo vijana 11 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), askari 1 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na dereva walipoteza maisha, na jumla ya watu 25 wakajeruhiwa, majira ya mchana baada ya ajali kutoka katika mteremko wa Mwansekwa uliopo Mjini Mbeya.
Aprili, watu wanane waliokuwa kwenye gari ndogo aina ya Toyota Noah walifariki dunia papo hapo baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi katika eneo la Igodima. Gari hilo lililokuwa likitokea Chunya kwenda Mbeya mjini, lilikuwa na abiria tisa waliokuwa wakienda katika msiba wa ndugu yao.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna msaidizi Musa Athumani Taib ameambia BBC kwamba uchunguzi zaidi bado unaendelea kujua chanzo cha ajali hiyo ya Jumapili.
Akitoa salamu za rambi rambi kufuatia ajali hiyo, Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema amesikitishwa na taarifa ya ajali hiyo
Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu, Rais Magufuli amewataka viongozi wa Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi na Mamlaka nyingine zinazohusika katika udhibiti wa usalama wa barabarani kujitafakari na kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na ajali hizo
''Inauma sana kuwapoteza idadi hii kubwa ya Watanzania wenzetu katika ajali za barabarani ambazo tunaweza kuziepuka. Nawapa pole familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo vya Watanzania wenzetu hawa, sote tuwaombee Marehemu wapumzishwe mahali pema peponi na majeruhi wapone haraka," amesema Rais Magufuli katika taarifa hiyo.